Kwa mujibu wa kitengo cha tarjuma cha shirika la habari la Hawza, Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki katika tamko lake imelaani vikali shambulio la utawala wa Kizayuni dhidi ya ujumbe wa mazungumzo wa Hamas huko Doha.
Matini kamili ya tamko hilo ni kama ifuatavyo:
“Tunalaani vikali shambulio lililofanywa na Israel dhidi ya ujumbe wa mazungumzo wa Hamas katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
Kushambulia ujumbe wa mazungumzo wa Hamas huku mazungumzo ya kusitisha vita yakiendelea, kunadhihirisha kuwa Israel haitafuti amani bali inalenga kuendeleza vita.
Kwa shambulio hili, Qatar ambayo inabeba jukumu la upatanishi katika mazungumzo ya kusitisha vita, nayo pia imeongezwa katika orodha ya nchi ambazo zimekuwa shabaha ya mashambulio ya Israel katika eneo hili, hali hii ni ushahidi wa wazi wa sera za upanuzi wa Israel katika eneo na kuufanya ugaidi kuwa sera rasmi ya kiserikali.
Tunasimama pamoja na Qatar dhidi ya shambulio hili la khiyana lililolenga mamlaka na usalama wa nchi hiyo.
Kwa mara nyingine tena tunaihimiza jumuiya ya kimataifa iwawekee Israel shinikizo la kusitisha uvamizi wake unaoendelea Palestina na katika ukanda huu kwa jumla.”
Maoni yako